Wednesday, August 31, 2016

HABARI ZA HIVI PUNDE:MANDAMANO YA UKUTA YAAHIRISHWA


CHADEMA yatangaza kuahirisha ‘Operesheni UKUTA’ hadi Oktoba Mosi kutoa nafasi ya mazungumzo kati ya Rais na viongozi wa Dini. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amesema maandamano ya UKUTA yameahirishwa kwa mwezi mmoja hadi tarehe Oktoba Mosi.

Aidha Mhe. Mbowe amesema “Tumepata wakati mgumu kufikia uamuzi, sio kila wakati viongozi tutafanya mambo yatayowapendeza wanachama wetu. Viongozi wa dini awali walikuja na ajenda moja, kuomba wabunge wa UKAWA warejee bungeni. Kamati kuu ya CHADEMA imepokea kwa heshima sana wito wa viongozi wa dini”.

Freeman Mbowe asema wamekutana mara nyingi kwenye vikao na Viongozi wa Dini lakini CCM imekuwa ikigoma kudhuria vikao hivyo.

1 comments: