Kipa wa Yanga, Yaw Berko.
Na Khatimu NahekaKIPA wa Yanga, Yaw Berko, amejiweka matatizoni katika kuwania namba kwenye kikosi hicho, kufuatia kubainika kusababisha matatizo makubwa kwenye michezo iliyopita.
Berko ambaye ni raia wa Ghana, awali alikuwa akiaminika kwa umahiri wake akiwa golini, kiwango ambacho sasa kimeporomoka, kufuatia kushindwa kuisaidia safu ya ulinzi ya kikosi hicho, kutokana na kiburi na tabia ya kususa.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha wa Makipa wa Yanga, Mfaume Athuman, alisema Berko ameshuka kiwango, tatizo ambalo limesababishwa na mambo mawili makubwa, ambayo ni kiburi na tabia ya kususa.
Mfaume ambaye aliwahi kuidakia timu hiyo miaka ya nyuma, alisema Berko amechangia kwa kiasi kikubwa kuyumba kwa safu ya ulinzi ya Yanga katika mechi za hivi karibuni huku akishindwa kuacha tabia ya kususa na kiburi.
Kocha huyo wa makipa alisema amepanga kumshauri kocha mkuu Ernest
Brandts kumweka benchi kuanzia mchezo wa leo dhidi ya Polisi Morogoro
utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na nafasi yake
itachukuliwa na Ally Mustapha ‘Barthez.’
“Inawezekana mabeki wakawa na matatizo, lakini yeye ndiye anatakiwa kusahihisha makosa yanayofanywa na mabeki, ukiangalia katika mechi iliyopita, mabao yale mawili ya harakaharaka tuliyofungwa na Ruvu (Shooting) alikuwa na uwezo wa kucheza zile krosi lakini akasusa na tukafungwa.
“Nimekuwa nikizungumza naye (Berko) kuhusu kuacha tabia hiyo ya kususasusa, lakini hata mazoezini kuna wakati amekuwa akifanya mazoezi kwa kiburi, jambo ambalo siyo sahihi.
“Utagundua kuwa ameanza maringo, lakini sasa nitazungumza na kocha mkuu na akikubali uamuzi wangu, ataanza kukaa benchi kuanzia mchezo wa keshokutwa (leo) ili ajue kwamba hatakiwi kusumbua mipango ya timu,” alisema Mfaume akionyesha kukasirishwa na tabia hiyo.

0 comments:
Post a Comment