Kocha wa Manchester United, Alex Ferguson
LONDON, ENGLAND
WAKATI Kocha wa Manchester United, Alex Ferguson akipanga kumtema Rio Ferdinand kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Braga leo Jumanne Chama cha Wachezaji wa Kulipwa, PFA kimekuja juu na kumwambia kocha huyo: "Usithubutu kumwadhibu Ferdinand."
Ferguson amepanga kumwadhibu Ferdinand kufuatia kosa la kukataa kuvaa fulana ya kupinga ubaguzi wa rangi 'Kick it Out' kwenye mechi dhidi ya Stoke wikiendi iliyopita lakini uongozi wa PFA umesema kila mtu ana nafasi ya kusimamia anachokiamini.
Jumamosi jioni Ferguson alitamka kuwa atahakikisha anamwadhibu mchezaji huyo na ataanza kwa kutokumpanga kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wachezaji, Clark Carlisle alisema kocha huyo akitoa adhabu atakuwa amekiuka haki za binadamu.
Manchester United itakuwa ugenini kupambana na Braga leo Jumanne huku ikiwa na historia nzuri katika ligi, lakini macho ya watazamaji yataangalia iwapo Ferdinand atapangwa au la.
Ingawa Braga nayo haijapoteza mechi tano za ligi, kikosi cha Ferguson kwa sasa ni kikali hasa baada ya Robin van Persie na Wayne Roooney kuonyesha ushurikiano.
Tayari Manchester United ina pointi sita kwenye Kundi H baada ya kuwafunga Galatasaray CFR Cluj na katika mechi za awali.
Katika mechi nyingine ya kesho Jumatano, Real Madrid kuifuta Borussia Dortmund kusaka ushindi. Real ni miongoni mwa timu sita zilizoshinda mechi mbili za kwanza nyingine ni Barcelona, Porto, Arsenal, Manchester United, BATE Borisov na Malaga.
Nazo Manchester City, Chelsea na Juventus zinahitaji ushindi kwa hamu kubwa ili kujiweka vizuri.
Mabingwa wa Serie A, Juventus hawajafungwa michezo 10 ya mashindano yote msimu huu, wametoka sare mechi mbili za kwanza za Kundi E, lakini wanatakiwa kushinda leo Jumanne wakiwa ugenini dhidi ya Nordsjaelland.
Mabingwa watetezi Chelsea watakuwa ugenini kuwavaa Shakhtar Donetsk leo Jumanne mchezo ambao unawakutanisha vinara wote wakiwa na pointi nne.
Manchester City, wenye pointi moja katika Kundi D watakuwa wageni kwa Ajax Amsterdam kesho Jumatano.
Ajax imeyumba kiuchumi na imekuwa ikifanya vibaya dhidi ya vigogo wengine wa Ulaya. Vile vile Barcelona itakuwa na mtihani dhidi ya Celtic.

0 comments:
Post a Comment